JUA SOKO LAKO KWANZA.

 Iliuweze kumhudumiamteja wako vizuri na kwa ufanisi ni muhimu sana kuwa  na ufahamu 

wa saikolojia ya mteja. Kumbuka saikolojia yamteja ndio inamwongoza mteja katika kufanya maamuzi yakununua/kulipia

bidhaa fulani nakuachana nabidhaa nyingine. 

Katika mada hii tutaangalia maeneo muhimu yanayoshikilia saikolojia yamtejawako.

HATUA 5 KABLA MTEJA HAJANUNUA

Nimuhimu kujua kuwa hadi mteja ametoa pesa yake mfukoni nakukupatia nimchakato mkubwa sanaa mbao lazima uweze kuufahamu kwani kila hatua inayo husika inaweza kuathiri maamuzi yake ya kutumia huduma/bidhaa yako. 

1: TAMBUA MAHITAJI YAKE 

Katika hatuahii mteja anafanya tathmini yauhitaji alionao ambao anajaribu kuutafutia suluhisho.

Hapa mteja anajishawishi kujua haswa tatizo lake nilipi.

Kama mtoahuduma nimuhimu sana kujua uhitaji

ambao mteja haswa ndio kipaumbele chake.

2: TAFUTA TAARIFA ZINAZO MUHUSU 

Baada ya kujua uhitaji wake,kinachofuata ni kuanza kutafuta taarifa zawatu au mahali ambapo tatizo alilonalo linaweza kutatuliwa. Hapa anaweza kutumia njia mbalimbali kamavile kutafuta kwenye mtandao, kuuliza marafiki au kutembelea sehemu ambazo huduma zinatolewa.

Hii inamaanisha ni muhimu sana kuhakikisha kuwa jinalako kamamtoa huduma linakuwa midomoni mwa watu au linapatikana katika mitandao n.k.

Kumbuka yule ambaye watu wengi wana msema vizuri ndiye atakaye shawishi zaidi mteja mpya kwenda kwake.

Nia kubwa katika hatua hii ni kupata watu mbalimbali ambao wanatoa huduma ili kuwajua kwa undani. Ni muhimu kwa mfanyabishara yeyote kupata taarifa za

kina kuhusu njia ambazo wateja wake wengi walimfahamu.

Je, walikufahamu kupitia marafiki, mitandao ya kijamii n.k hii itakusaidia kuweka mikakati yako ya masoko vizuri zaidi. 

Kesho tutaendelea na somo hili usikose.




Emmanuel Jacob Lohay 

Mtaalam wa soft skills & Enterprineurship

Email: sse751775@gmail.com

Facebook: soft skills & Enterprineurship 

Phone:+255782751775  +255752751775









Comments

Popular posts from this blog

Utangulizi

UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI?

USIKURUPUKE MJASIRIAMALI