UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI?
Kila mmoja anatamani kuwa mjasiriamali, changamoto ni kuwa mjasiriamali katika nini?
Chamuhimu kabla hujawa mjasiriamali, unapaswa kutumia muda wakutosha kufanya utafiti juu ya tatizo lililopo na uone namna ya kulitatua...... Ujasiriamali sio kuuza nguo, viatu, vipodozi, karanga, mahindi ya kuchoma/kuchemsha, mbogamboga, vyombo, NK.... yaani kiufupi mjasiriamali sio mmachinga wala mfanyabiashara ndogondogo. Mjasiriamali ni mgunduzi wa tatizo na akigundua lazima atafute utatuzi wa hilo Tatizo,Huyu sio mfanya biashara.
TOFAUTI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA.
✓ Mfanyabiashara:
Ni mtu au Kampuni inayo nunua bidhaa fulani sehemu (A) na kwenda kuiuza ikiwa vile vile sehemu (B) Ikiwa atanunua sh. 1000 yeye ataweka gharama zake za usafiri na gharama zingine zilizo tumika hadi kupata Bidhaa hiyo, na kisha ataweka na faida juu yake kisha atakwenda kuuza sehemu (B) sh 2500. Kumbuka hiyo bidhaa haijaongezewa thamani yeyote kama ni nguo anaiuza kama ilivyo au Sukari, Chumvi, Mafuta,kiberiti, Sabuni, Mshumaa Soda, Maji, Nk. Huyu ndie mfanya biashara.
Lakini pia tofauti nyingine namna wanavyo waza au wanavyopata wazo la Biashara, huyu Mfanyabiashara yeye anaanza kujiuliza "Hivi Biashara gani inalipa? Na inahitaji niwe na shilingi ngapi ili niweze kuifanya?" Anatafuta hela anapanga chumba anaagiza mzigo anaanza kuuza bila kufanya utafiti wa wateja wake na washindani wake wa kibiasha. Mwisho wa siku huishia kuuza kidogo sana na kushindwa kuendesha biashara huishia kufilisika.
MJASIRIAMALI:
Huyu yeye haanzi kujiuliza juu ya biashara gani inalipa yeye hujiuliza kuna changamoto gani katika jamii inayo nizunguka au kikundi cha watu wenye changamoto zinazo fanana.
Akigundua hilo hutafuta namna ya kutatua hiyo changamoto na anapo tatua hiyo changamoto atapata pesa. Utofauti uliopo ni kwamba yeye haanzi kuwaza pesa bali huanza kuwaza tatizo na suluhisho lake kisha hela ni matokeo ya utatuzi wa hilo tatizo, inaweza kuwa kuuza bidhaa fulani au kutoa huduma fulani, NIKWAMBIE UKWELI KUNA HUDUMA NYINGI MNO KWENYE JAMII LEO AMBAZO WALA HAZIHITAJI KUWA NA PESA, NI KUWA NA WAZO TU NA WATU WATAKULIPA PESA NYINGI SANA.....
TAFSIRI YA BIASHARA NI NINI?
Ni utatuzi wa tatizo fulani katika jamii.
Sio kuuza bidhaa kama wengi wetu wanavyo elewa.
Ni mimi Mr Emmanuel Jacob
Mtaalam wa Soft Skills ad Enterprineurship
Phone: +255782 751 775 +255752 751 775
email: sse751775@gmail.com
P. O. BOX 833 Mwanza Tanzania
Comments
Post a Comment