Utangulizi
Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha katika blog hii ambayo ninaamini kuwa utajifunza mambo mengi kuhusu maswala ya ujasiriamali.
Ninajua umesikia sana juu ya ujasiriamali kwa kila namna, na inawezekana umeufanyia majaribio lakini pia inawezekana umeona mafanikio fulani yakitokea katika huo unaonutambua kama ujasiriamali.
Lakini hapa utajua mjasiriamali ni mtu wa sifa zipi au ni mtu wa namna gani? Lakini pia utaweza kuwatofautisha mjasiriamali na mfanyabiashara. Hizi dhana mbili watu wamekuwa wakizichanganya sana, mjasiriamali anatambulika kama mfanya biashara na mfanya biashara anatambulika kama mjasiriamali.
Lakini pia katika Blog hii utajua namna ya kufanya utafiti wa kijasiriamali, labda nianze kwa kukuambia mapema tu kuwa Mjasiriamali ni mtafiti na mgunduzi pia, yeye hupata pesa kutokana na ugundizi wake na huo ugundizi humuingizia pesa. Nafikiri hapo umeanza kujiuliza maswali sasa ......yaani mjasiriamali ni mgunduzi Ahahaaaaaa!!!!!!!!!!!!
Ndio ni Mgunduzi ambaye hugundua tatizo na kulitafutia ufumbuzi na watu wenye hilo tatizo hulipa pesa ili kuondokana na tatizo hilo.
Nataka nikuambie happ ulipo kuna fursa nyingi zimekuzunguka ambazo unaweza kuzifanya na ukaingiza pesa, najua utashangaa sana kusikia hivyo. Narudia tena ziko fursa nyingi hapo unapoishi, hapo Ofisini kwako, au jamii yako inayo kuzunguka, hapa tutakusaidia kutoa Tongotongo au ukungu ulioko mbele yako ili uone hizo fursa na uzigeuze kuwa pesa.
Yako mambo mengi ya kujifunza kabla ya kuanza ujasiriamali, na nimalize kwa kusema Ujasiriamali ni Ajira inayo lipa.
Tafadhali endelea kutembelea blog hii kwa kujiongezea maarifa na ujuzi wa kijasiriamali.
Ni mimi Mr Emmanuel Jacob
Mtaalam wa Soft skills & Entrepreneurship.
Phon: +255782 751 775/ +255752 751 775
Email: sse751775@gmail.com
Comments
Post a Comment