USIKURUPUKE MJASIRIAMALI

 Leo hii Mtanzania akisikia elimu ya ujasiria mali mawazo yake yanaenda kwenye kujifunza kutengeneza sabuni, Mishumaa, Batiki NK. Lakini hawazi juu ya masoko yaani kama nitatengeneza Sabuni nitamuuzia nani na kwa bei gani, hilo huwa hatuwazi kabisa matokeo yake tunatengeneza sabuni na hatuna pakuziuzia tunakata tamaa ya kuendelea na hiyo biashara.


Na ukisikia kunamtu anafundisha masomo ya ujasiriamali unasema ni wale wale sasa ngoja nikuibie siri ya kufanikiwa katika Ujasiriamali.


1. Jifunze na ujue nini maana ya ujasiriamali.

2. Baini tatizo lililopo katika jamii ya watu unao taka kufanya nao biashara au huduma fulani.

3. Tambua uwezo wao kifadha na wadhifa wao katika jamii 

4. Elewa rika lao /umri wao 

5. Elewa muda wao wanao fanya manunuzi, au namna wanavyo nunua.

6. Vitu gani vinawavutia 

Inawezekana kwa sasa  unafanya biashara au unatoa huduma fulani ila matokeo yake si sawa na juhudi unazo ziweka, najua hata wewe hujaridhika na matokeo yake. 

 lakini ikiwa utafanya biashara au kutoa huduma kwa kuzingatia vigezo hivi ninakuhakikishia utakuwa na wateja wa uhakika na kipato cha uhakika.


Ahsante sana: 


Mr Emmanuel Jacob Lohay 

Mtaalam wa:  SOFT SKILLS  AND ENTREPRENEURSHIP.

Phone:+255782 751 775 +255752 751 775

email: sse751775@gmail.com










Comments

Popular posts from this blog

Utangulizi

UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI?