Posts

Showing posts from July, 2023

JUA SOKO LAKO KWANZA.

 Iliuweze kumhudumiamteja wako vizuri na kwa ufanisi ni muhimu sana kuwa  na ufahamu  wa saikolojia ya mteja. Kumbuka saikolojia yamteja ndio inamwongoza mteja katika kufanya maamuzi yakununua/kulipia bidhaa fulani nakuachana nabidhaa nyingine.  Katika mada hii tutaangalia maeneo muhimu yanayoshikilia saikolojia yamtejawako. HATUA 5 KABLA MTEJA HAJANUNUA Nimuhimu kujua kuwa hadi mteja ametoa pesa yake mfukoni nakukupatia nimchakato mkubwa sanaa mbao lazima uweze kuufahamu kwani kila hatua inayo husika inaweza kuathiri maamuzi yake ya kutumia huduma/bidhaa yako.  1: TAMBUA MAHITAJI YAKE  Katika hatuahii mteja anafanya tathmini yauhitaji alionao ambao anajaribu kuutafutia suluhisho. Hapa mteja anajishawishi kujua haswa tatizo lake nilipi. Kama mtoahuduma nimuhimu sana kujua uhitaji ambao mteja haswa ndio kipaumbele chake. 2: TAFUTA TAARIFA ZINAZO MUHUSU  Baada ya kujua uhitaji wake,kinachofuata ni kuanza kutafuta taarifa zawatu au mahali ambapo tatizo al...

USIKURUPUKE MJASIRIAMALI

  Leo hii Mtanzania akisikia elimu ya ujasiria mali mawazo yake yanaenda kwenye kujifunza kutengeneza sabuni, Mishumaa, Batiki NK. Lakini hawazi juu ya masoko yaani kama nitatengeneza Sabuni nitamuuzia nani na kwa bei gani, hilo huwa hatuwazi kabisa matokeo yake tunatengeneza sabuni na hatuna pakuziuzia tunakata tamaa ya kuendelea na hiyo biashara. Na ukisikia kunamtu anafundisha masomo ya ujasiriamali unasema ni wale wale sasa ngoja nikuibie siri ya kufanikiwa katika Ujasiriamali. 1. Jifunze na ujue nini maana ya ujasiriamali. 2. Baini tatizo lililopo katika jamii ya watu unao taka kufanya nao biashara au huduma fulani. 3. Tambua uwezo wao kifadha na wadhifa wao katika jamii  4 . Elewa rika lao /umri wao  5. Elewa muda wao wanao fanya manunuzi, au namna wanavyo nunua. 6. Vitu gani vinawavutia   Inawezekana kwa sasa  unafanya biashara au unatoa huduma fulani ila matokeo yake si sawa na juhudi unazo ziweka, najua hata wewe hujaridhika na matokeo yake.  ...

UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI?

 Kila mmoja anatamani kuwa mjasiriamali, changamoto ni kuwa mjasiriamali katika nini? Chamuhimu kabla hujawa mjasiriamali, unapaswa kutumia muda wakutosha kufanya utafiti juu ya tatizo lililopo na uone namna ya kulitatua...... Ujasiriamali sio kuuza nguo, viatu, vipodozi, karanga, mahindi ya kuchoma/kuchemsha, mbogamboga, vyombo, NK.... yaani kiufupi mjasiriamali sio mmachinga wala mfanyabiashara ndogondogo. Mjasiriamali ni mgunduzi wa tatizo na akigundua lazima atafute utatuzi wa hilo Tatizo,Huyu sio mfanya biashara. TOFAUTI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA. ✓ Mfanyabiashara: Ni mtu au Kampuni inayo nunua bidhaa fulani sehemu (A) na kwenda kuiuza ikiwa vile vile sehemu (B) Ikiwa atanunua sh. 1000  yeye ataweka gharama zake za usafiri na gharama zingine zilizo tumika hadi kupata Bidhaa hiyo, na kisha ataweka na faida juu yake kisha atakwenda kuuza sehemu (B) sh 2500. Kumbuka hiyo bidhaa haijaongezewa thamani yeyote kama ni nguo anaiuza kama ilivyo au Sukari, Chumvi, Mafuta,ki...

Utangulizi

  Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha katika blog hii ambayo ninaamini kuwa utajifunza mambo mengi kuhusu maswala ya ujasiriamali. Ninajua umesikia sana juu ya ujasiriamali kwa kila namna, na inawezekana umeufanyia majaribio lakini pia inawezekana umeona mafanikio fulani yakitokea katika huo unaonutambua kama ujasiriamali. Lakini hapa utajua mjasiriamali ni mtu wa sifa zipi au ni mtu wa namna gani? Lakini pia utaweza kuwatofautisha mjasiriamali na mfanyabiashara. Hizi dhana mbili watu wamekuwa wakizichanganya sana, mjasiriamali anatambulika kama mfanya biashara na mfanya biashara anatambulika kama mjasiriamali. Lakini pia katika Blog hii utajua namna ya kufanya utafiti wa kijasiriamali, labda nianze kwa kukuambia mapema tu kuwa Mjasiriamali ni mtafiti na mgunduzi pia, yeye hupata pesa kutokana na ugundizi wake na huo ugundizi humuingizia pesa. Nafikiri hapo umeanza kujiuliza maswali sasa ......yaani mjasiriamali ni mgunduzi Ahahaaaaaa!!!!!!!!!!!!  Ndio ni Mgunduzi ambaye ...